• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 25 October 2016

    MD KAYOMBO AMUAGIZA AFISA MTENDAJI KUSIMAMIA MAPATO YA SOKO KWA UAMINIFU

    Afisa Mtendaji wa Kata ya Mburahati Jijini Dar es salaam ametakiwa kusimamia kwa
    uaminifu mapato ya soko Mburahati ili kuimarisha mapato ya Manispaa hiyo ambayo
    yataimarisha uboreshaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
    Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg
    John Lipesi Kayombo wakati alipofanya ziara sokoni hapo kwa lengo la kujionea
    hali halisi ya soko pamoja na hali ya ukusanyaji wa mapato.
    Sambamba na agizo hilo pia Mkurugenzi amemtaka Afisa Mtendaji huyo kwa kushirikiana na kamati ya soko Kuandaa orodha ya
    majina ya walipaji wote pamoja na kiasi wamachotakiwa kulipa, kutolewa namba
    pamoja na kuwepo na orodha ya kiasi kinachotakiwa kukusanywa kutoka katika
    maduka hayo, Kutoa mapendekezo mapya ya viwango vya tozo, na kuwepo na jina la
    kila mmiliki wa meza sokoni hapo na kiasi cha ushuru anacholipa.
    MD Kayombo ametoa siku tano kwa Afisa Mtendaji
    huyo kwa kumtaka Kuwasilisha orodha ya watu wote wanaodaiwa tozo na kodi katika
    soko na vibanda pamoja na muda wanaodaiwa sambamba na Kutengeneza data base ya
    wafanyabiashara wote katika soko hilo.
    Pamoja na ukaguzi huo Mkurugenzi alipata maelezo juu ya ukusanyaji mapato
    katika soko la Mburahati lililopo pembeni ya jengo la soko linalojengwa. Akisomewa taarifa ya soko hilo na katibu wa soko Ndg Fikiri Pazi alisema kuwa wenye meza hulipa
    kiasi cha shs 200 kwa siku na wenye vibanda (maduka)hulipa shs21000 kwa mwezi
    viwango ambavyo wamekuwa wakilipa tangu kuanza kwa soko hilo mwaka 1982.
    Mkurugenzi hakuridhika na viwango hivyo kwa ni ni viwango vilivyopitwa na
    wakati kutokana na hilo ameagiza tozo hizo ziangaliwe upya na walete
    mapendekezo ya viwango vipya ambapo menejimenti ya Manispaa itavipitia na
    kulinganisha na mapendekezo ya viwango vya menejimenti na kisha kufanya maamuzi
    ya viwango vipya.
    Akiendelea kutoa taarifa alisema mashine ya kukatia risiti imeharibika hiyvyo
    kusababisha ushuru kutokusanywa tangu 6/10/2016,baada ya kusikia hayo
    Mkurugenzi ameagiza apate jumla ya kiasi kilichotakiwa kulipwa na kumtaka
    kufuatilia pesa hizo na ziingizwe kwenye akaunti mpya ya Manispaa ya Ubungo na
    kuwasilisha slip ya benki ofisi za Manispaa.
    Pamoja na ukaguzi wa soko Mkurugenzi alikagua pia Zahanati ya Mburahati
    iliyopo katika kata hiyo na kujionea kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati hiyo na
    kutoa maagizo yakufanyika usafi  ili
    Zahanati hiyo ianze kufanya kazi na kuhudumia wananchi.
    Kwa upande wake Diwani wa Kata Mburahati Mhe Yusufu Yenga amemshukuru
    Mkurugenzi huyo kwa kuwatembelea na kujionea hali halisi na changamoto
    zilizopo.
    Diwanihuyo alisema kuwa NdgKayombo ni Mkurugenzi wa kwanza kufika hapo kwa
    ajili ya kujionea hali halisi ya ukusanyaji wa mapato na ziara ya kikazi katika
    eneo hilo ambapo Ameahidi kumpa ushirikiano na kumuunga mkono katika juhudi
    zake za kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Halmashauri yake.
    Mkurugenzi huyo ameahidi kurudi tena katika eneo hilo akiwa na timu ya
    waandisi wanaosimamia ujenzi wa soko hilo kwa ajili ya ukaguzi zaidi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI