Manchester United wanaikaribisha Manchester City leo katika mchezo wa raundi ya nne ya Kombe la Ligi maarufu kama EFL, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Old Trafford.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na upinzani unaochangizwa na uhasama wa makocha wote wawili kwani kuna kipindi walifikia kutopeana hata mikono wakati wakiwa La Liga Jose Mourinho alikuwa anakinoa kikosi cha Real Madrid na Pep Guardiola akiwa Barcelona timu hizo zimekuwa na upinzani mkubwa hivyo wanakutana tena Uingereza hii ikiwa ni mara ya pili ya kwanza ilikuwa kwenye Liga Mourinho alikubali kichapo cha magoli 2-1 toka kwa Guardiola.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na upinzani unaochangizwa na uhasama wa makocha wote wawili kwani kuna kipindi walifikia kutopeana hata mikono wakati wakiwa La Liga Jose Mourinho alikuwa anakinoa kikosi cha Real Madrid na Pep Guardiola akiwa Barcelona timu hizo zimekuwa na upinzani mkubwa hivyo wanakutana tena Uingereza hii ikiwa ni mara ya pili ya kwanza ilikuwa kwenye Liga Mourinho alikubali kichapo cha magoli 2-1 toka kwa Guardiola.
City hawashinda michezo mitano kwenye michuano yote na meneja wao Pep Guardiola ataendelea kufanya mabadiliko ya kikosi chake.
“Baadhi watacheza leo. Nahitaji kuona wachezaji mazoezini halafu ndiyo natoa maamuzi yupi acheze na yupi asicheze,” amesema Guardiola
United pia mwezi huu bado hawaonja ladha ya ushindi kwenye ligi mwezi huu ikiwa ni pamoja na kupewa kipigo cha aibu cha magoli 4-0 kutoka kwa Chelsea Jumapili, lakini Guardiola amesema “mara zote amekuwa akiwaheshimu wapinzani wake”
“Ni timu yenye ubora wa hali ya juu. Tumewazidi alama, ikiwa ni sawa uwiano wa michezo miwili tu,” amesema Guardiola ambaye kwenye mchezo wa Premier League waliokutana mwezi September alishinda 2-1.
“Michezo ya mahasimu ina uzito wa kipekee. Tutajaribu kucheza kwa umakini wa hali ya juu ili kupata matokeo.”
Guardiola ameongeza kwa kusema kuwa angependa kuona mshambuliaji wake raia wa Argentina Sergio Aguero, ambaye amekuhuwa akihusishwa na kuhama klabuni hapo akibaki kwa muda mrefu zaidi”.
“Nina furaha sana na Sergio. Ningependa kumwona anabaki na kuendelea kucheza pamoja nasi. Ni mchezaji wa aina yake,” Guardiola amesema.
Dondoo za Mechi kwa timu hizo:
Manchester United wameshinda mechi mbili tu Kombe la ligi kai ya sita zilizopita dhidi ya Manchester City (sare 1, kufungwa mara 3), japokuwa hawajapoteza mechi tatu walizokutana Old Trafford.
Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana kwenye Kombe la Ligi ilikuwa ni msimu wa 2009-10 kwenye nusu fainali ambapo United walishinda kwa wastani wa magoli 2-3, baada ya kushinda 3-1 Old Trafford.
Mara zote ambazo Man City wamewaondosha mahasimu wao mashindanoni kwenye Kombe la Ligi, wamefanikiwa kubeba kombe hilo (1969-70 na 1975-76).
Kwenye michuano yote, Man City wameshinda mechi nne kati ya sita zilizopita katika Uwanja wa Old Trafford (sare 1, kufungwa mara 1).
Ushindi mara mbili kati ya tatu wa Jose Mourinho dhidi ya Pep Guardiola kama meneja umetokana na mechi za michuano ya ligi (mara moja kwenye Champions League, na mwingine kwenye Kombe la Copa Del Rey).
Kwenye michuano yote, Guardiola ameshindwa kupata matokeo kwenye mechi tatu za ugenini akiwa na Man City. Amewahi kucheza mechi nne za ugenini bila ushindi katika historia ya maisha yake ya ukocha (ilikuwa ni mwezi March 2009).
No comments:
Post a Comment