
Msafara wa Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI ukiwasili kwenye viwanja vya Ikulu ambapo amepokelewa na Mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli na kufanya naye mazungumzo kabla ya kushuhudia kusainiwa kwa mikataba zaidi ya 20 ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili Ikulu jijini Dar es salaam.
Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wa Morocco pia ameahidi kujenga msikiti mkubwa hapa jijini Dar es salaan na pia kujenga uwanja mkubwa wa michezo mkoani Dodoma hayo yamesemwa na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati akimshukuru mfalme huyo kwa kukubali ombi hilo.
(PICHA – IKULU NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakipita katika gadi ya mapokezi iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakilakiwa na wafanyakazi pamoja na wageni mbalimbali katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakielekea kusalimiana na viongozi mbalimbali wakati Mfalme huyo alipowasili kwenye viwanja vya Ikulu.

Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VIakisalimiana na viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ikulu ambapo amepokelewa na Mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Maguful.

Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VIakiongozwa na Mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufulikuelekea Ikulu.

Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI akipunga mkono wakati akilakiwa na mamia ya wananchi Ikulu alipowasili na kupokelewa Mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli

Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI akiangalia vikundi vya ngoma havipo pichani wakati alipowasili kwenye viwanja vya Ikulu ambapo amepokelewa na Mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli

Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VIakipiga ngoma pamoja na Mwenyeji wake Rais Dk. John Pombe Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Taaswira ya Kinyago alichomkabidhi mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIC Mwanaidi Shemweta kushoto na Melania Razaro Mwanasheria wa NIC wakisubirikuingia Ikulu kwa ajili ya kushuhudia utiwaji wa saini wa mkataba wa Shirika la Bima la Morocco naTanzania

Waziri wa Nishati na Madini Mh. Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Cliford Tandari kulia na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Bima NIC Sam Kamanga na kulia ni mbunge wa jimbo la Kwimba Shanif Mansoor .

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Cliford Tandari akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk. Florence Turuka ikulu jijini Dar es salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa Bw. Sam Kamanga akiwa pamoja na baadhi ya wageni waalikwa wakiingia ikulu.

Elisante Maleko Kaimu Mkurugenzi wa Masoko NIC kulia Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIC Mwanaidi Shemweta kushoto na Melania Razaro Mwanasheria wa NIC wakiingia Ikulu.

Baadhi ya wageni wakiwa Ikulu kwa ajili ya kushuhudia utiwaji saini wa mikataba ya kibiashara kati ya Tanzania na Morocco.

Kutoka kulia ni Oktavian Mshiu Makamu wa Rais wa Viwanda TCCIA , KV Choudary Mkurugenzi wa Lake Oil , Khaled Mohamed Hassan Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Lake Group na Thobias Laizer Mshauri wa Masuala ya Sheria wakiwa katika hafla hiyo.

Kutoka kulia ni Geofrey Meena Meneja wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB, Philip Chitaunga Mkurugenzi wa Masoko TTB na baadhi ya Maofisa wa bodi hiyo wakiwa katika hafla hiyo.

Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi akiwa pamoja na wageni waalikwa wengine katika hafla hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa NIC Bw. Sam Kamanga akiwa katika hafla hiyo.

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justine Mtalikwa,Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi na Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo Bw. Thomas Samkyiwakisubiri kutia saini mikataba ya taasisi zao.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIC Mwanaidi Shemweta katikati, Melania Razaro Mwanasheria wa NIC kushoto ni Elisante Maleko Kaimu Mkurugenzi wa Masoko.

Baadhi ya wageni walioongozana na Mfalme wa VI wa Morocco wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la ATCL Bw. Ladslaus Matindi akiteta jambo akiteta jambo na mmoja wa waalikwa katika hafla hiyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Lake Group Bw. Ally Awadh akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Super Doll Group Bw. Seif wakati wa utiwaji saini wa mikataba ya kibiashara kati ya Makampuni Tanzania na Morocco.

Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandali akizungumza na baadhi ya wakuu wa vitengo wa kituo hicho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufulina mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VIwakishuhudia utiwaji saini wa mikataba ya kibiashara kati ya Tanzania na Morocco Ikulu leo.

Ujumbe wa wafanyabiashara na maofisa wa serikali ulioongozana na Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI ukiwa katika hafla hiyo.

Wakuu wa mashirika mbalimbali wakitiliana saini mikataba mbalimbali ya kibiashara kati ya serikali na mashirika ya Tanzania na Morocco.

Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la ATCL Bw. Ladslaus Maindi akibadilisha na mkataba na mmoja wa wakuu wa shirika la ndege la Morocco.

Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi akisaini mkataba huku Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akishuhudia.

Wakuu wa mashirika mbalimbali wakitiliana saini mikataba mbalimbali ya kibiashara kati ya serikali na mashirika ya Tanzania na Morocco.
No comments:
Post a Comment