• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 17 October 2016

    Serikali imeyasainisha mikataba ya kujiendesha kwa faida Mashirika 12 ya Umma.......Yatakayojiendesha kihasara kuchukuliwa hatua.


    Taasisi na Mashirika ya Umma nchini yametakiwa kujiendesha kwa faida huku yakiwa na mtazamo wa kiushindani na makampuni yaliyo chini ya sekta binafsi na kwamba hakuna sababu yoyote kwa mashirika hayo kuendeshwa kwa hasara na kugeuka mzigo kwa serikal

    Msajili wa Hazina nchini Bw. Lawrence Mafuru ametoa agizo hilo janajijini Dar es Salaam wakati akisaini makubaliano ya kiutendaji na taasisi 12 za umma, mkataba unaohusisha malengo ya uendeshaji, namna ya kuhudumia wananchi sambamba na usimamizi bora wa rasilimali za umma zilizopo ndani ya mashirika hayo.

    Zoezi hilo la linafanya idadi ya taasisi ambazo msajili wa hazina amesaini nazo makubaliano kufikia thelathini tangu aanze utaratibu huo unaoendana na falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji katika taasisi na mashirika ya umma.

    Katika maelezo yake Bw. Mafuru amesema haikubaliki kuona makampuni na taasisi za umma zikiendelea kupata hasara kwa kutekeleza majukumu yale yale ambayo taasisi na makampuni binafsi yanapata ufanisi na faida pasipo visingizio vyovyote.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI