• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 19 October 2016

    Siku ya Kimataifa ya kutokomeza Umasikini ilivyofana


    Kila siku ya tarehe 15 Oktoba, Dunia nzima huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umasikini, ambapo mwaka huu  kauli mbiu ya  siku hiyo ilikuwa ni
    ‘’KUTOKA UDHALILISHAJI NA UTENGWAJI MPAKA USHIRIKISHWAJI ‘’.
    Mtandao wa Dini mbalimbali kwaajili ya watoto ulimwenguni  uitwao Global Network of Religion for Children (GNRC-Tanzania) wamefanikiwa kuhitimisha siku hii kwa namna ya pekee kabisa ambapo tangu tarehe 15 Oktoba wamekuwa wakiandaa matukio mbalimbali yaliyolenga kuwajengea uwezo watoto haswa wa Shule za msingi kwa kuandaa mashindano tofautitofauti kama Midahalo na Michezo ikiwa na lengo la  kuwajengea watoto uwezo (capacity building)  na kuwapa elimu ambayo itaweza kuwakomboa katika janga la umasikini .
    mix1
    Wanafunzi wa shule ya Msingi  Oysterbay wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baraka Chedego kutoka GNRC -Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu
    mix2
    wanafunzi wakiwa katika mdahalo
    mix3
    Vainess Mbaga  Ofisa Elimu  akitoa elimu kwa watoto
    mix4
    Washiriki wa Mdahalo wakisalimiana na Mama Joyce Mdachi kutoka GNRC na viongozi wengine wa shule
    mix6
    Mfano wa vyeti walivyotunukiwa wanafunzi kutoka na ushiriki mzuri wa siku hii ya kipekee.
    mix5

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI