• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 19 October 2016

    STAND YAANZA KUPEPESA, MAJIMAJI MWENDO WA USHINDI TU.


    standdd1
    Kikosi cha timu ya Stand United ya Shinyanga.
    ………………………………………………………………..
    Kwa mara ya kwanza timu ya Stand United imeshindwa kuendeleza rekodi ya kupata ushindi mfululizo baada ya kujinjwa na wenyeji Tanzania Prisons magoli 2-1 mchezo wa Ligi Kuu Vodacom mzunguko wa kumi na moja kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
    Matokeo haya yanaashiria kuwa mzimu wa Pratrick Liewig ambaye ameachana na timu hiyo kwa kushindwa kumlipa haki zake za mshahara na tangua aondoke Stand alikuwa bado hajapoteza mchezo wowote msimu huu.
    Licha ya kupoteza mchezo huu bado wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 21 na Prisons imekuwa timu ya kwanza kuifunga Stand ya mkoani Shinyanga.
    Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam watoto wa jiji hilo timu ya African Lyon imeshindwa kutamba mbele ya wageni Majimaji baada ya kupokea kichapo cha magoli 2-0.
    Ushindi huu ni watatu kwa Majimaji ambayo msimu huu ilianza vibaya kwa kufungwa mechi saba mfululizo na baada ya kumleta Kocha Ongola mpaka sasa timu hiyo ina pointi 9 na kushika kuwaacha Toto African wakiwa wanashika mkia kwa alama 8.
    TAZAMA MATOKEO YA MECHI NYINGINE:
    .Toto African 0-2 Yanga
    .T.Prisons 2-1 Stand United
    .Ruvu 1-1 Mwadui FC
    .Lyon 0-2 Majimaji
    .Ndanda FC 1-1 Mbeya City.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI