Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika CAF limetangaza makundi manne ya Michuano ya kombe la AFCON itakayofanyika nchini Gabon mwakani kwa kushirikisha jumla ya mataifa 16 kuwania ubingwa huo.
Katika ukanda wa Afrika Mashariki itawakilishwa na timu ya Uganda the Cranes ambayo imewekwa kundi la kifo kutokana na vigogo ambao inachuana nao kuwania ubingwa unaoshikiliwa na mabingwa watetezi Ivory Coastal.
Hata hivyo Uganda wakijipanga vizuri wanaweza kufanya maajabu kwani hata kwenye michuano ya kufuzu kombe la Dunia mwaka 2018 wapo kundi moja na Ghana pamoja na Misri.
Ghana na Uganda zilitoka suluhu kwenye mchezo wa ufunguzi wa Kundi E kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 na wanatarajia kucheza mara mbili dhidi ya Misri baada ya michuano ya AFCON kumalizika.
TAZAMA MAKUNDI YALIVYOPANGWA:
GROUP A:
Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea Bissau.
GROUP B:
Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe.
GROUP C:
Cote D’Ivoire, DR Congo, Morocco, Togo.
GROUP D:
Ghana, Mali, Egypt, Uganda
No comments:
Post a Comment