• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 22 October 2016

    WAPIGWA MSASA KUHUSU KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE, USUBI, KICHOCHO, TRAKOMA

     Ofisa Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar Kaitaba akielezea umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha umma kujenga tabia ya  kutumia Kingatiba ya magonjwa ya kichocho, Minyoo ya Tumbo, Usubi Matende na Mabusha wakati wa Warsha iliyoshirikisha wanahabari, Dar es Salaam leo. Kampeni ya kuwapatia wananchi Tibakinga kwa wakazi takribani mil. 4 wa Jiji la Dar es Salaam itaanza Oktoba 25 waka huu. 
     Meneja Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Upendo Mwingira akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
     Wanahabari wakiwa katika warsha hiyo
     Mtangazaji wa BBC, Halima Kassim akitafakari jambo  kuhusu semina hiyo ya wanahabari kupata uelewa kuhusu magonjwa hayo na jinsi ya kuwaelimisha wananchi kutumia Kingatiba kwa kumeza  dawa mara noja kila mwaka ili kuboresha afya
     Mtaalamu Kaitaba akionesha baadhi ya dawa za Kingatiba ya magonjwa hayo
     Ofisa Habari wa Mradi huo, Said Makora akiwataka wanahabari kuwaelimiasha wananchi juu ya magonjwa hayo na jinsi ya kupata Kingatiba kwa kuandika makala, habari, majarida na kutumia mitandao ya kijamii kwa nia ya kuyatokomeza magonjwa hayo kufikia mwaka 2020.
     Kaitaba akionesha vifaa vinavyotumika kuwapima watu ili wapewe dawa kulingana na kimo chake.
     Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Jasmin akichangia mada wakati wa semina hiyo.
     Wana habari wakipatiwa dawa za Kingatiba za magonjwa hayo
    Mtangazaji wa E FM Radio akipimwa urefu ndipo apatiwe dawa 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI