Wataalamu wa mifugo na uvuvi hapa nchini wametakiwa kujiwekeza katika kujiendeleza ili kuweza kuwafikia wafugaji waweze kuzalisha kwa tija na kuachana na ufugaji wa mazoea unaoharibu mazingira.
Akizungumza Naibu waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Wiliam Ole Nasha wakati akifunga mkutano wa 39 wa wataalamu wa mifugo na uvuvi kutoka kwenye halmashauri zote hapa nchini na vyuo vikuu vya Sokoine na Mandela na kushirikiasha wataalamu kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika.
Nasha alisema kuwa ili kuwekeza na kuweza kupata tija kwa wafugaji na wavuvi hakuna budi wataalamu hao kuzitumia taaluma zao kwa ufanisi kwa kuweza kuwafikia wafugaji na wavuvi kwa wakati ilikukabiliana na changamoto wanazokutana nazo.
“lengo lenu la mkutano huu la kujadili masuala kadhaa ya kitaalamu lijikite pia kujadili masuala ya Tabianchi kwani yamekuwa yakiendana na hali nzima ya uvuvi na ufugaji katika kuimarisha uzalishaji bora bila kusahau Teknolojia ya kisasa”alisisitiza Ole Nasha.
Aidha akizungumza wakati akimkaribisha Naibu waziri Mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa mifugo na uvuvi hapa nchini dkta. Daniel Kamwihangilo alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa siku tatu ni kujadili mambo kadhaa ya kitaalamu ya watumiaji wa mifugo na uboreshaji, kuimarisha uzalishaji wa mifugona uvuvi.Teknolojia mbali mbali za uendeshaji wa mifugo na uvuvimiongoni mwa wazalishaji. Na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi katika uzalishaji wa mifugo hapa nchini ili kuongza thamani ya mazao hayo.
Alisema kuwa ilikufikia uzalishaji bora unaohitajika hakuna budi maofisa ugani wote hapa nchini wakawa na mamlaka ya udhibiti ilikuondoa wataalamu wasio na tija katika kuhakikisha sera nzuri zinaweza kuleta tija katika kufikia malengo tarajiwa.
“Kupitia mkutano huu tunalaani mauuaji ya watafiti wa kilimo yaliootokea mkoani Dodoma bila kusahau mapigano ya wafugaji na wakulima hapa nchini kwani yamekuwa yakirudisha nyuma maendeleo ya sekta yetu sisi kama wataalamu tunaendelea kulaani matukio ya aina hiyo”alisema dkta Kamwihangilo.
No comments:
Post a Comment