
Waziri wa maliasili na Utalii nchini Prof. Jumanne Magembe amewataka watendaji wa chuo cha utalii cha Taifa kuweza kukiendesha kwa faida na kutokutegemea ruzuku kutoka serikali kuu.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea moja ya idara anazozisimamia katika wizara yake Prof. Magembe amesema, ni vema chuo hicho kiweze kuboresha mitaala yake ikiwa ni pamoja na kuendana soko la utalii nchini, kwani sekta hiyo imekuwa ni kitovu kikubwa cha uchumi na mapato kwa taifa.

Hata hivyo Prof. Magembe amesema kuwa ni ajabu kuona baadhi ya hoteli nchini zenye nyota tano zikiwa hazina wafanyakazi wazalendo wa kitanzania badala yake wanachukua wafanyakazi kutoka nje ya nchi, pia amesikitishwa na kitendo cha chuo hicho kutokuwa na mazingira yasiyoridhisha ingawa wana kila kitu kinachotakiwa kufanyika kuwa cha kisasa.
Aidha waziri Magembe ameshangazwa na kitendo cha bodi hiyo kutothamini sekta ya utalii ambayo imeonekana kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 500,000 huku walio nje na walio jiajili wenyewe kuwadumia watalii ni 1,200,000 hata hivyo amesisitiza kuwa sekta hiyo kiini chake kipo kwenye katika sekta binafsi.
Katika hatua nyingine Waziri Magembe amewataadhalisha watendaji wa chuo hicho kujitathimini kwa kutoigemea serikali kwa kuililia kupewa ruzuku na kuwafananisha sawa na machungwa yaliyowekwa mahala pasipokuwa pa kwake.
“wakati tunaanza kujenga chuo hiki, tulichimba msingi mimi na waziri wa ushirikiano wa kimataifa wa ufaransa wakati huo nilipata bahati ya kuwa waziri wa maliasili na utalii, lakini malengo yetu yalijikita kwenye eneo moja kwamba tutafundisha wataalam wenye ujunzi, wataalam wa sekta ya utalii.”
Wakati huohuo amekitaka chuo hicho kutobadiri malengo yake ya kutoa wataalam na badala yake waache mara moja kujifanya kuwa wakala wa sekta ya utalii na mahoteli nchini. “Kuanzia sasa hiki chuo siyo wakala ni chuo cha Utalii cha Taifa.”
No comments:
Post a Comment