• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 24 October 2016

    WAZIRI WA MAMBO YA NJE AWATAKA VIJANA WACHANGAMKIE FURASA ZA AJIRA UN

    NA Z4NEWS BLOG/TV

    Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki balozi Augustine mahiga amesema ushirikiano wa Tanzania na umoja wa mataifa (UN)  wataendeleza ulinzi wa amani katika mataifa mbalimbali kama wanavofanya kwa Sudan ya kusini.

    Akizungumza katika hafla ya kusherehekea miaka 71ya umoja huo Dar es salaam , balozi Mahiga amewataka  Vijana  nchini  kuchangamkie fursa za ajira zinazopatikana katika umoja huo.   

       Amesema mikakati wanayoiweka kwenye suala la ujenzi wa viwanda litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana wanaomaliza masomo yao katika vyuo mbalimbali nchini.    

             " siasa yetu ya kutofungamana katika upande wowote itazidi kuboresha  misingi ambayo itaendelea kuheshimiwa ikiwa ni pamoja na utu' haki za binadam.


        Amesema mikakati wanayoiweka kwenye suala la ujenzi wa viwanda litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana wanaomaliza masomo yao katika vyuo mbalimbali nchini.     
           
    Ameongeza kuwa suala la amani na ulinzi vitaendelea kudumishwa ikiwamo na Vijana walioko mashuleni kuendelea kufundishwa ili waweze kuelewa umoja wa mataifa kwa undani.

    Sherehe za miaka 71 za  umoja  wa mataifa zimehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa huku suala la ulinzi ' pamoja na amani likiwa limepewa kipaumbele kwa  mataifa mbalimbali

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI