WAZIRI wa Fedha , Mipango na Uchumi Zanzibar Khalid Salim amesema kuwa asilimia ya wananchi wanaosihi katika umaskini wa chakula imepungua kwa asalimia 11.7 kutokana na utafiti 2009-2010 hadi aslimia 10.8 katika mwaka 2014-2015.
Alifahamisha kuwa taarifa zaidi zinasema kwamba pato la mwananchi pia limeongezeka ambapao kiashiria kikubwa ni kuimarika kwa huduma za kijamii ikiwemo maji , afya , umeme , elimu pamoja na mawasiliano .
Waziri Khalid alisema Serikali imekuwa ikitekeleza mikakati madhubuti ya kupambana na umaskini kwa lengo la kuboresha hali za maisha za wananchi wake pamoja na kuchochea fursa za kiuchumi ili kushusha kiwango cha umaskini katika kaya.
Alisema pamoja na mafanikio hayo , bado Serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha kwamba wananchi wanaondokana na umaskini na kuishauri jamii kuchagua miradi ambayo itasaidia moja kwa moja katika kuwaletea kipato katika familia zao .
“Utafiti uliofanywa mwaka 2009-2010 umeonyesha kupungua kwa asmilika ya maskini wa chakula kwa wananchi na kwamba Serikali itaendelea kuboresha mazingira ili kutoa fursa zaidi kiuchumi ”alifahamisha .
Aidha waziri alipongeza juhudi zinazochukuliwa a wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati katika kujikomboa na umaskini na kuwataka kuongeza ubunifu ili kuboresha bidhaa zao na kufanya ziingie kwenye ushindani wa soko .
Mapema mwakilishi wa wajasiriamali Bi Sifuni alisema pamoja na wananchi waliokubali kujiajiri wenyewe lakini bado changamoto kubwa ni ukosefu wa soko la uhakikisha la kuuzia bidhaa wanazozalisha .
Aidha Sifuni alisema kwamba tabia ya baadhi ya wananchi ya kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wan chi ya nchi nayo ni changamoto inayowakabili na kuwataka wananchi kutambua kwamba bidhaa za ndani zinaubora sawa na nje .
“Tunazochangamoto nyingi na iwapo zitapatiwa ufumbuzi wajasiriamali tunaweza kupunguza kwa aslimia kubwa umaskini wa kipato na chakula katika kaya , changamoto ambazo zinachangiwa na baadhi ya wananchi kutothmini bidhaa zetu ”alieleza.
Akimkaribisha Waziri Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman alisema kwamba wananchi wa Wilaya ya Micheweni hususani wanawake wamekuwa msitari wa mbele katika kujiletea maendeleo kupitia sekta mbali ikiwemo kilimo na ufumaji .
Alisema tofauti ilivyokuwa miaka ya nyuma , wanawake wa Wilaya hiyo na Mkoa wa Kaskazini Pemba wamehamasika na kujiunga pamoja kwenye vikundi vya uzalishaji mali baada ya kupokea taaluma kutoka kwa mashirika na maafisa wa ushirika wa Serikali .
No comments:
Post a Comment