Kituo cha
msaada wa sheria kwa wanawake WLAC kimeitaka serikali kurekebisha sheria ya
mirathi ya kimila kwa kuwa sheria iliyopo ni ya kibaguzi na kandamizi kwa
wanawake na wototo wa kike hali inayochangia kurudisha nyuma jitihada na maendeleo
yao katika kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamebainishwa
leo jijini dar-es-salaam na mkurugenzi wa kituo cha msaada wa sheria kwa
wanawake bi,Theodosia Nshala na kueleza
kuwa sheria ya mirathi na kimila ni ya
kuwakandamiza wanawake na watoto na inakinzana na katiba ya jamhuri ya muungano
wa Tanzania kwa kuwa zinashikilia mila na desturi ambazo zinamnyima mjane na mtoto
wa kike fursa ya kurithi na kuongeza mashauri ya mirathi.
‘’tatizo la
mirathi bado ni kubwa na Linahitaji jitihada madhubuti ilikuweka mazingira
rafiki kwa upatikanaji wa haki kwa wajane na watoto ikiwemo kuwepo kwa sheria
ya mirathi inayosimamia haki za wanawake na watoto hivyo tunaiomba serikali
kubadilisha sheria hii kandamizi kwa wajane. alisema Theodosia.
Mkurugenzi
huyo alifafanua kuwa idadi ya mashauri 811 ya mirathi yamefikishwa
kwa wasaidizi wa kisheria katika mikoa ya iringa, kigoma,rukwa katika kipindi
cha mwezi januari hadi oktoba 2016 huku mkoa wa mbeya ukiongoza kwa kupokea
mashauri 153 ya mirathi.
Hata hivyo
aliongeza kwa kusema kuwa maamuzi ya Mahakama yameendelea kugharimu maisha ya
wajane na watoto wa kike kwakuwa bado upatikanaji wa haki za mirathi umekuwa mgumu
japo mahakama inatumia busarana nguvu nyingi katika kuhakikisha haki
inapatikana
.


No comments:
Post a Comment