• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday 29 November 2016

    MAKONDA AMWAGIZA SIRO KUWATIA NDANI MAFISA

    Na Ahmed Kombo
    MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda,amemwagiza Ofisa Ardhi wa mkoa huo,Edgar Japhet andike orodha ya Maofisa wa ardhi wa Kinondoni wote waliohusika katika mchezo mchafu wa kutoa hati feki
    apeleke majina yao kwa Kamishina Simoni Siro ili wakamatwe.


    Tamko hilo Makonda,lilitolewa jana eneo la Mabwepande Kinondoni wakati wa kuitisha ziara yake ya siku kumi.

    "Maofisa ardhi wa Kinondoni wababaishaji nitawashugulikia  amuwezi kuuza   maeneo ya wananchi kwa hati feki ofisa ardhi fatilia majina yote kesho yaani leo  mpaka saa kumi wawekwe ndani."alisema Makonda.

    Makonda alisema maofisa ardhi  wote kiama chenu kimefika nitawashughulikia mmoja baada mmoja  ili Dar es Salaam iweze kuwa safi kuondoa kero za wananchi wote wapate huduma  jamii vizuri.

    Alisema bora awe Mkuu wa mkoa wa siku moja kuliko miaka 20 yeye kama mkuu wa mkoa huo atakikisha wananchi wake kero zao zinapata ufumbuzi katika mitaa yao Watendaji watazitatua.

      Makonda Jana ameitimisha ziara yake ya Siku kumi,kwa kusikiliza kero zao  zikiwemo kero zilizokithiri za migogoro ya ardhi.

    Katika hatua nyingine  Makonda amepiga marufuku mnada kuwepo eneo LA soko LA Kawe Wilayani humo badala yake wameambiwa watatafutiwa eneo lao na Mkuu wa Wilaya.
    Alisema soko LA Kawe libaki kuwepo eneo lake ili kingize mapato halmashauri hiyo.

    Makonda alifanikiwa kusikiliza kero 663 na amezipatia ufumbuzi zaidi ya kero 400.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI