• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 7 November 2016

    MECHI TATU ZA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA ZAAHIRISHWA

    mwadui-fcZile mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara za raundi ya Nane Duru la Kwanza, sasa  Jumatano.
    Michezo hiyo inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC ambayo ilipewa jina la Mechi Na. 57 itachezwa Uwanja wa CCM Kambarage wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezon Na. 60 Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ilihali Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na.59.
    Mechi zilipangiwa ratiba, lakini tarehe zake hazikupangwa (TBA). Tayari Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imewasiliana na wahusika kuhusu mabadiliko hayo. Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI