Habari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Zavala kata ya Buyuni Ilala, Chiku Said baada ya kutuhumiwa kuuza viwanja vya watu pamoja na serikali kinyume na sheria.
Baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kuuza viwanja vya serikali kinyume na sheria bila kuwahusisha wajumbe wenzake hali ambayo imesababisha mgogoro mkubwa wa ardhi katika eneo hilo.
Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa huyo kumtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela kuthibitishwa kuuzwa kwa eneo hilo kinyume na sheria.
“Mkuu wa mkoa, ni kweli tulikuwa na eneo block J lakini limeuzwa,” alisema afisa huyo “Nataka kuwaambia kitu mwenyeviti wa mtaa hawaruhusiwi kuuza eneo katika mtaa. Mimi ningewataka wenyekiti kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kuepuka kutokea kwa hayo mambo,”
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi kuhusu swala hilo
No comments:
Post a Comment