..

Friday, 25 November 2016
Habari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemtaka Diwani wa kata ya Ubungo ambaye ni Meya Mteule wa Manispaa hiyo Boniphace Jacob kuhakikisha anamaliza changamoto ya madarasa matano katika shule ya Sekondari Urafiki.
RC Makonda ameyasema hayo wakati anazindua shule hiyo ya urafiki ikiwa ni moja ya muendelezo wa ziara ya siku 10 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
RC Makonda amesema viongozi wa kisiasa inabidi waache siasa za ujanja ujanja na badala yake kuwatumikia wananchi.
"Diwani wa hapa anatakribani miaka mitano hivyo inabidi apambane na kuhakikisha uhaba wa vyumba hivyo vitano unakamilika"
katika hatua nyingine RC Makonda amewataka wanafunzi kujitahidi kusoma masomo ya Sayansi ili waweze kuingia katika soko la ushindani wa ajira kwa vitu vingi vimetawaliwa na Sayansi.
Home
Habari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul amemtaka Diwani wa Ubungo ambaye ni Meya kutafuta wawekezaji
No comments:
Post a Comment