..
Monday, 14 November 2016
Habari
Watanzania wamehimizwa kuondoa fikra kutegemea kuajiriwa baada ya kumaliza masomo ya elimu juu bali wametakiwa kufikiria mbinu za kujiajiri kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wasiopungua elfu 1000 waliohitimu vyuo mbali mbali na kanda nyinginezo za elimu ndani ya wilaya hiyo, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kubuni biashara na miradi mbalimbali.
Hapi amesema serikali haina uwezo wa kuajiri wanafunzi wote kutokana na ufinyu wa ajira hivyo anawataka kubuni mipango ya kujiajiri.

No comments:
Post a Comment