Mwenyekiti soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mokiwa Hassani ameomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba
Mwenyekiti akijitetea mbele ya Wananchi
Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuuwa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni siku ya chache za ziara yake katika jiji la dar es salaam
Kufuatia kesi hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti wa soko hilo Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo na kufafanua kuwa bei hiyo ya shilingi laki nne kwa kizimba ni makubaliano kati yao na wananchi hao, pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuendesha soko hilo, ambalo bado halijakabidhiwa kwa Halmashauri.
Kufuatia utetezi huo ikamlazimu Mkuu wa Mkoa kutumia busara ambapo ameuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kusimamia uundwaji wa uongozi wa soko hilo haraka mpaka kufikia mwezi Desemba kero zinazolikabili soko hilo ziwe zimetatuliwa
No comments:
Post a Comment