• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 4 November 2016

    TAASISI YA ANSAF YAWANOA WADAU WA KILIMO KANDA YA ZIWA

    Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoani Mwanza, Joanen Kukwami akifungua mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
     
    Mkutano huo uliandaliwa na Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuhakikisha kunakuwa na kilimo chenye tija katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili familia ziweze kujikimu kiuchumi na kichakula.
    Na BMG
    Wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa wakimsikiliza Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoani Mwanza, Joanen Kukwami wakati akifungua mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
    Meneja Mradi wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Diana Lugano, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
    Wadau wa kilimo wakimsikiliza Meneja mradi wa ANSAF wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
    Mratibu na Mchambuzi wa Sera na Bajeti kutoka Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Joseph Nyamboha, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
    Mratibu na Mchambuzi wa Sera na Bajeti kutoka Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, Joseph Nyamboha, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
    Jimmy Luhende ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini, akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Kilimo Kanda ya Ziwa.
    Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza, akijitambulisha.
    Washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
    Washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
    Washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza.
    Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza akichangia mada.
    Mmoja wa washiriki wa mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza akichangia mada.
    Picha ya pamoja
    ************************************************
    Upungufu wa
    maafisa kilimo pamoja na uuzaji wa mbegu zisizo na ubora katika mikoa ya kanda
    ya ziwa umeelezwa kusababishwa sekta ya kilimo katika mikoa hiyo kuzorota.
     
    Hayo
    yalibainishwa jana Jijini Mwanza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo uliolenga kujadili
    namna bora ya kuboresha sekta hiyo.
     
    Walisema
    baadhi ya maafisa kilimo waliopo katika mikoa ya kanda ya ziwa kushindwa
    kuwafikia wakulima na kuwapatia elimu ya kilimo husababisha kilimo kisicho na
    tisha huku uuzaji wa mbegu za kilimo zisizoota ukikwamisha kabisa juhudi za
    wakulima kulima zao hilo.
     
     
    Mkutano huo
    uliandaliwa na Jukwaa la wadau wa kilimo nchini ANSAF na kuwakutanisha wadau
    mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima, viongozi wa serikali pamoja na taasisi
    binafsi ambapo pamoja na mambo mengine umeadhimia kufikisha elimu kwa wakulima
    ili kulima kilimo chenye tija.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI