..

Sunday, 27 November 2016
Habari
Wakazi wa Kibamba Wilayani Ubungo wamezuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Paul Makonda huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kuwa wamedhulumiwa ardhi yao.
Akizungumza na wakazi hao waliokuwa wamesimamisha msafara huo Mkuu wa Wilaya hiyo Humphrey Polepole amewataka wakazi hao kufuata utaratibu Kwani madai yao yamefika mezani kwake na baadhi yamenza kushughulikiwa kwa watu kulipwa fidia zao kutokana na kupisha eneo la chuo na hospitali ya MUHAS .
DC Polepole amesisitiza kuwa serikali ipo pamoja na wAjax hao ambao wengine wanadai fidia ya eneo la kwembe na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alihaidi kuwa watalipwa, vilevile Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alihaidi kuwa serikali itazifanyia kazi ahadi zote zilizoachwa na serikali iliyopita.
DC Polepole ameongeza kuwa kwa wale wakazi waliopo maeneo ya hifadhi ya barabara serikali itaendelea na msimamo wake wa upanuzi wa barabara kama alivyohaidi Rais Magufuli jana kwenye Mkutano wa hadhara wa RC Makonda uliofanyika Maramba Mawili.
No comments:
Post a Comment