
Waziri wa Afya, MaendeleoyaJamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu wa pili kulia akipokea Dubini ya kufanyia operesheni ya macho kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Standard Chartered Bw. Sanjay Rughani watatu kushoto wakati wa kukabidhi vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 300.2 leojijini Dar es salaam, wa kwa kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wizara Dkt. Mohammed Mohammed.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Kifaa cha uchunguziwa macho Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Daisy Majamba kulia wakati wa kukabidhiana vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 300.2 leojijini Dar es salaam.

Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kukabidhiana vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 300.2 leojijini Dar es salaam.

Baadhi ya vifaa vya uchunguzi wa macho vilivyokabidhiwa kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kutoka kwa Benki ya Standard Chartered na Shirika lisilo la kiserikali CBM vyenye thamani ya shilingi milioni300.2.
Picha Na Ally Daud-Maelezo
No comments:
Post a Comment