Kutoka kushoto ni mratibu wa mradi Michael Maurius, katikati Kanali mstaafu Idd Kipingu, na mwisho Meneja Masoko wa Kampuni ya New Habari Corp ltd Michel Bugaira.walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari jana
IKIWA tunaelekea katika uenyeji wa michuano ya Soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019, Kanali Idd Kipingu kupitia Shule yake ya Lord Baden Powell, imeandaa mchuano wa kupata vijana 20 watakaosoma na kucheza mpira bure katika Shule hiyo.
Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam mratibu wa mradi huo Michael Maurus, alisema jumla ya vijana 150 wamejitokeza katika mchuano huo, unaotarajia kuanza Januari 1 hadi 3 katika viwanja wa Shule hiyo.
‘’Mbali na maandalizi ya michuano hiyo , lakini mradi huo ni mahususi kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya vijana wanaomaliza darasa la saba kujiunga na shule hiyo’’, alisema.
Kanali mstaafu Kipingu alisema kuwa, vijana wanaotakiwa katika Shule hiyo ni wale wenye umri wa miaka 13 na 14, ambao mpaka michuano hiyo ya vijana ikifika watakuwa wameshakomaa.
‘’Tunataka vijana wenye vipaji, ni jambo la aibu kuona Tanzania tunakuwa wenyeji wa michuano ya vijana, alafu tunashuhudia kombe likiondoka machoni kwetu, hii sasa basi, tunaanza maandalizi mapema’’, alisema.
Kipingu alisema kuwa, katika mchuano huo kutakuwa na wataalamu mbali mbali, wakiwemo makocha wa timu za vijana wa Simba, Yanga na Azama, ambao watafanya kazi kazi ya kuwachuja vijana hao ili wabakie 20 wanaotakiwa.
Shule hiyo ya kipingu ilianza mwa 2008, ni Sekondari kama zilivyo nyingine isipokuwa shule hii ni kiskauti, pia imekuwa ikiiibua vipaji na kuwaingiza shuleni hapo
No comments:
Post a Comment