Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe ametoa salamu za rambirambi kwa Wahanga wa shambulio lililofanywa na nchi yake katika Bandari ya Pearl, nchini Marekani, miaka sabini na tano iliyopita.
Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa kwenye kituo cha jeshi la majini la Marekani akiwa sambamba na mwenyeji wake Rais Barak Obama, Bwana Abe amekiri kukosa la kusema kutokana na uzito wa ziara yake katika kumbukumbu ya wale wote waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo.
Ameishukuru Marekani kwa uvumilivu wake na kuongeza kuwa kitisho cha vita hakitajirudia kamwe.
Naye Rais Obama kwa upande wake ameitaja ziara hiyo ya Waziri mkuu wa Japan kuwa ni ya kihistoria na kusema kuwa inakumbusha kuwa hata maumivu makubwa yaliyotokana na vita yanaweza kuleta urafiki na amani ya kudumu.
Amesema baada ya vita mahusiano yao yamekuwa ya amani na nchi zilizokuwa katika ukanda wa Asia Pacifik.
Miezi saba iliyopita viongozi hao wawili walitembelea pia mji wa Japan, Hiroshima, ambako Marekani uliushambulia kwa mabomu ya nyuklia
No comments:
Post a Comment