Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka wakurugenzi wa Manispaa mbalimbali nchini kutekeleza miradi mbalimbali ya serikali kwa bei nafuu na kwa viwango, bila kuweka maslahi yao binafsi jambo ambalo limekuwa likikwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naibu Waziri huyo ametoa maagizo hayo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa majengo ya shule ya msingi Kisutu chini ya ufadhili wa BAPS CHARITIES ambao wamefanya ukarabati kwa shilingi milioni 50, jambo ambalo limempelekea Naibu Waziri Jafo kuwataka wakurugenzi kuiga mfano huo.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Jafo amewataka wazazi, walimu na wanafunzi kuilinda na kuitunza miundombinu hiyo iliyokarabatiwa kwa lengo la kuendelea kuboresha wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki.
No comments:
Post a Comment