Habari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo amekutana na ugeni kutoka nchi ya China Jimbo la Jiang Su, Manispaa ya xuzhou na kukubalina mambo mbalimbali yenyetija kwa maendeleo ya Wilaya ya Ilala.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam DC Mjema amesema kuwa ugeni huo unatija kwao kwani miongoni mwa mambo waliokubaliana ni kuipendezesha wilaya ya Ilala ifanane na maeneo mbalimbali ya nchini China kwa kuzingatia usafi wa maeneo husika, vilevile wamekubaliana katika suala la usalama kwa kupeana ujuzi wa kiusalama wanaotumia China kwa mfano vifaa vya kisasa wanavyotumia kudhibiti vitendo vya uhalifu na kulinda miji yao.
Huku suala lingine walilokubaliana na wadau hao DC Mjema amelitaja kuwa ni suala la elimu hususani ya Sayansi kwa malengo mahususi ya kuchochea Tanzania ya Viwanda aliyokuwa anainadi Rais Magufuli kipindi cha kampeni za urais, na kusisitiza kuwa yapo maeneo mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji.
Katika hatua nyingine DC Mjema ameeleza kuwa China ilikuwa sawa na Tanzania miaka 20 iliyopita lakini nidhamu na bidii ya kufanyakazi ndiyo imewapelekea kufika hapo walipo, hivyo amewaomba watanzania kuiga mfano huwa ili kufikia malengo ya mapinduzi ya kiuchumi.
Vilevile kwa upande wake muwakilishi kutoka wa wadau kutoka China Zhang Aijun amesema wapo tayari kushirikiana na wilaya ya Ilala na wataleta wataalaamu kuangalia fursa nyingine ambazo wanaweza kuwekeza kwa maendeleo ya pande zote mbili.
No comments:
Post a Comment