Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kuwa mabalozi wema wa maadili kwa kufanya kazi kwa maslahi ya umma na kutoweka mbele maslahi binafsi.
DC Mjema ameyasema hayo leo wakati akifungua semina ya mafunzo ya sheria ya uongozi wa maadili ya umma yaliyoandaliwa na Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma kwa ajili ya madiwani ambapo amefafanua kuwa madiwani ndiyo wasimamizi wa shughuli zote za maendeleo za Manispaa ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo hivyo wakizingatia maadili maendeleo kwa wananchi yatapatikana.
Pia DC Mjema ameeleza kuwa madiwani inabidi wawe wakweli kwa kuweka wazi mali wanazomiliki, huku akiongeza kuwa maadili yao yasiwe kwenye mali pekee bali hata kwenye tabia kwa kufanya matendo mema ya mfano wa kuigwa kwenye jamii, ikiwemo kuacha ulevi na tabia zenye kufanana na hayo.
No comments:
Post a Comment