• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 5 December 2016

    Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala ameeleza kuwa asilimia 90 ya wanawake walioathiriwa na matukio ya ubakaji


    Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ameeleza kuwa asilimia 90 ya wanawake walioathiriwa na matukio ya ubakaji wanawafahamu wahalifu wao, lakini waathirika hao wamekuwa hawatoai ushirikiano wa kutosha.

    Katibu Tawala huyo ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wilaya ya Ilala, yenye kaulimbiu ya "Funguka, Pinga Ukatili wa Kijinsia Elimu Salama kwa Wote" na kueleza kuwa matukio mengi ya ukatili yanatokea kwenye familia na wahusika wanajuana jambo linalopelekea kutozifikisha taarifa hizo mahala husika na hata kama wakizifikisha huzikana kesi hizo na kutozitolea ushahidi, jambo ambalo linachochea kuendelea kwa vitendo hivyo.

    Katibu Tawala huyo amewataka wazazi kuwa waangalizi wa watoto wao ikiwemo kutowaruhusu kwenda kwenye vibanda vya video na kuachana na imani za kishirikina zinazowapelekea wazazi kuwaingilia watoto ili wawe matajiri, huku akisisitiza kuwa serikali imejipanga kutatua changamoto zinazochangia matukio hayo kuendelea ikiwemo umasikini, hivyo serikali imetenga asilimia 10 kupitia Halmashauri zote kwa ajili ya wanawake ili waweze kujikwamua.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI