Habari
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini, mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete ameiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza mbele ya mkuu wa mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Ridhiwani amesema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi pamoja na kijijini pasipo kufata taratibu za kisheria,jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo.
Kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini kuwa ombeni nanyi mtapewa, kilio cha mbunge Ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30, kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo. “Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi, haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa”, alisema Ndikilo.
RC Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo, licha ya wafugaji katika kijiji cha kitonga kudai kuwa wana ngombe wapatao laki 5, lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho, huku akimtaka mmoja wafugaji anayeonekana kuwa mbabe kijiji hapo aliyefahamika kwa jina moja la leki kuhakikisha anatii agizo la kuondoka ndani ya mwezi mmoja haraka iwezekanavyo.
Akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo. Kwaupande wake mbunge wa chalizne mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoiungia kinyemela.
Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo.
No comments:
Post a Comment