• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 3 December 2016

    Madhimisho ya siku ya walemavu duniani

    DAS Ilala: Wazazi DSM wanaongoza kutelekeza watoto wenye ulemavu 
    Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu katika mkoa wa Dar es Salaam wanadaiwa kuongoza kutelekeza watoto wao katika shule maalumu za walemavu hasa zilizopo katika wilaya ya Ilala.

    Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa Ilala, DAS Edward Mpogolo katika Maadhimisho ya  Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu yaliyofanyika Disemba 3,2016 katika viwanja vya MnaziMmoja.

    Mpogolo ameyasema hayo wakati akieleza changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu katika mkoa wa Dar es Salaam.


    "DSM ina shule za watu wenye ulemavu nne, 3 zipo Ilala. Wazazi na walezi hao wamekuwa wakiwapeleka watoto katika shule hizo kwa lengo la kupata elimu kisha kuwatelekeza," amesema.

    Ametaja changamoto nyingine zinazowakabili walemavu kuwa ni umasikini kutokana kwamba hakuna mfumo mzuri wa kuwawezesha kiuchumi na ubaguzi dhidi yao.


    "Changamoto nyingine ni ubovu wa miundombinu ya shule hizo sababu ni za kizamani zilijengwa muda mrefu, serikali tunaiomba itusaidie namna ya kuziboresha shule hizo ," amesema.

    : Serikali imesema itazifutia usajili taasisi na vyama vya watu wenye ulemavu ambazo hutumia watu wenye ulemavu kuomba misaada nje ya nchi pasipo kuifikisha misaada kwa wahusika.
    Kauli hiyo imetolewa Disemba 3,2016 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akizindua Kamusi ya Watu wenye ulemavu katika maadhimisho ya kimataifa ya siku ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika Kitaifa jijini Dar es Salaam.

    Mhagama ameitoa kauli hiyo baada ya Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Ummy Hamis kusema kuwa kuna baadhi ya taasisi zinazoshughulikia walemavu zinalidhalilisha Taifa kwa kuomba misaada nje ya nchi kwa kigezo cha kusaidia walemavu pasipo kuifikisha misaada hiyo kwa walengwa.

    " Naomba nikubaliane na wewe, kweli ziko taasisi zinazofanya hivyo na kudhalilisha taifa kwa kigezo cha kusaidia walemavu lakini hawafanyi hivyo. Tutazipembua taasisi zote kama zina saidia walemavu, zisizofanya hivyo tutazifuta bila kusita," amesema.

    Aidha, Mhagama amesema serikali itahakikisha walemavu wote nchini wanapata haki zao pamoja na kuwawekea mkakati wa kuwawezesha kiuchumi.
    "Katika mipango ya serikali inayopangwa hatuwezi kuacha kundi la watu wenye ulemavu,  tutaliwezesha ili litusaidie kupunguza umasikini," amesema.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI