Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira mh January Makamba, Leo amefanya semimina fupi na wahariri pamoja na waandishi wa habari kuhusu hali ya mazingira nchini na kueleza kuwa tatizo la uchafuzi wa mazingira nikubwa najuhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuinusuru nchi kugeuka kuwa jangwa .
Aidha Mh Makamba amesema kutokana na ziara yake ya aliyotembelea Mkoa 10 nchini ili kujionea hali ya mazingira nchini amejionea uharibifu Mkubwa wa vyanzo vya maji ambapo katika ziwa Rukwa limeathiwa na wakulia kina chake kinapungua kutoka mita 9 hadi 6. na safu za milima mbeya amekusudia kulitangaza kuwa eneo nyeti la uhifadhi mazingira na maeneo mengine nchini yanayofanana na hayo halmashauri zimeagizwa kuyawekea alama.
Katika mkutano huo limeibuka suala la uuzaji mkaa nje ya nchi ambapo waandishi wa habari wamemuomba Waziri kulitazama upya jambo hilo kwa kuwa linachangia kwa kiasi kikubwa ukataji wa miti.
Hata hivyo Mh Makamba amewataka wahalili na waandishi kuendelea kutoa Elimu kwa jamii juu ya kuhifadhi mazingira ikiwemo kupanda miti.
" Nimewaita Leo kuwaomba kuwaomba tusaidiane na kushirikiana kuifanaya nchi yetu na jamii yetu na watu wetu wayape kipaumbele masuala ya hifadhi ya mazingiza" amesema Makamba.
No comments:
Post a Comment