• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 4 December 2016

    Mchezaji wa Mbao fc afariki dunia uwanja wa Kaitaba


    ismail-khalfanMchezaji Ismail Khalfan amefariki dunia baada ya kugongana na beki wa Mwadui FC katika mchezo wa raundi ya saba ligi ya vijana (U-20) huko Bukoba mkoani Kagera.
    Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Z4news blog kutoka Bukoba, tayari imethibitishwa na daktari wa hospitali ya rufaa ya Bukoba kuwa, amefariki dunia na mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali hiyo.
    “Alianguka uwanjani ghafla baada ya kufanyiwa faulo mguuni akainama kushika mguu tukamuona ameshika kifua akaanguka chini lakini wakati anaanguka alikuwa peke yake”, ni maneno ya manager wa Mbao FC Bashiri wakati akizungumza na kituo kimoja cha radio cha mkoani Dar es Salaam.
    “Tukajaribu kumsaidia kumpatia huduma madaktari wa timu zote pamoja na msalaba mwekundu tukasaidiana kumpeleka hospitali.”
    “Wakati huo timu yetu ilikuwa ikiongoza kwa goli 1-0 goli lililofungwa na marehem Ismail Khalfan na jingine lilifungwa wakati mimi sipo nikiwa nimeenda hospitali.”

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI