Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametembelewa na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Harison Mwakyembe na kumuahidi kujenga mahakama za mwanzo 20 kwa kila wilaya ili kuchochea upatikanaji wa haki kwa haraka zaidi.
RC Makonda ameeleza kuwa watanzania wengi wamekuwa haki zao zimekuwa zinachelewa kutokana uchache wa mahakama, hivyo mahakama hizo zitaleta ahueni na kufafanua kuwa ule mpango wa kujenga vituo 20 vya polisi Dar es Salaam ambao umeisha anza utaenda sambamba na huo wa mahakama 20 kwa lengo la kuleta haki kwa wanyonge.
Kwa upande wake Waziri Mwakyembe amepongeza juhudi za Makonda kwa hatua hizo na kuhaidi kutoa ushirikiano wa kutosha huku akiwataka wakuu wa wilaya na mikoa ambao ndiyo wenyeviti wa kusimamia maadili katika mahakama kufanya kazi hiyo ipasavyo kwa kuunda kamati za maadili na kuwaripoti wale wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi zao
No comments:
Post a Comment