• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 16 December 2016

    MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AWAKABIDHI WANASHERIA KWA WAKUU WA WILAYA

    Wakazi wa jiji la dar-es-salaam wameombwa kutochukua hatua
    zozote zinazohusiana na sheria mpaka wapate ushauri kutoka kwa wanasheria ili kuondoa sintofahamu katika jamii.


    Mkuu wa mkoa wa dar Paul Makonda ametoa wito huo mapema leo wakati akiwatambulisha vijana wanasheria kwa wakuu wa wilaya zote za mkoa wa dar ambao watawasaidia katika kutatua migogoro mbalimbali.


    akitoa shukrani kwa niaba ya wakuu wa wilaya,mkuu wa wilaya ya temeke Felix Lyaniva amempongeza mkuu wa mkoa kwa maono hayo na kuelekeza kuwa kupatikana kwa wanasheria hao kutasaidia wananchi wenye uelewa mdogo katika jamii.

    akizungumza kwa niaba ya wanasheria bi Georgia Kamina amewaahidi wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu..katika hatua nyingine mkuu wa mkoa ametoa msaada wa shilingi laki mbili kwa andrew komba kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake alex komba anayesumbuliwa na uvimbe pamoja na kupooza mwili mzima huku akiahidi kumpa milioni moja kila mwezi.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI