
Lihundi alikamatwa Disemba 21 majira ya saa 8 mchana ambapo awali alifunguliwa shitaka la kuandika habari za uchochezi, ambalo hata hivyo katika hali ya sintofahamu leo asubuhi Disemba 22, polisi katika kituo cha Usariver walikanusha kwamba hakukuwa shitaka lolote isipokua wanafuata agizo la mkuu wa wilaya la kumuweka mahabusu.
Akizungumza mara baada ya kuachiwa kwa dhamana majira ya saa 9:30 alasiri Lihundi amesema katika mahojiano na askari wa upelelezi ametuhumiwa kuandika habari nyingi zinazohusu malalamiko ya wananchi bila kile kinachoelezwa kusikiliza upande wa uongozi wa wilaya.
Mwanasheria wa mwandishi huyo kutoka tume ya haki za binadamu Edwin Silayo amesema Lihundi ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 na wadhamini wawili huku akitakiwa kuripoti kituo hicho cha polisi Disemba ishirini na saba.
Tukio la kukamatwa kwa mwandishi huyu limewagusa waandishi wa habari vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa wa mkoa wa Arusha ambao wameonekana kusimamisha shughuli zao na kupiga kambi katika kituo hicho kwa siku zote mbili.
No comments:
Post a Comment