Mkuu wa mradi wa Agra, ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini-Dodoma, Dkt. Mark Msaki (kushoto), akitoa ufafanuzi
kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
(Katikati) wakati akikagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla
ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya
Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza. Kushoto kwa
Dkt. Kijaji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Mhe. Angelina Mabula (Mb).
Mwanafunzi wa kiume wa Stashahada Mwaka wa Pili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini, Kituo cha Mwanza, akielezea kuhusu mafunzo wanayoyapata chuoni
hapo na namna elimu hiyo inavyosaidia kuendeleza vijiji walivyokwenda
kufanya mazoezi kwa vitendo mkoani Mwanza, wakati Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Hayupo pichani) alipotembelea
na kukagua maonesho hayo ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na
chuo hicho.
Mwanafunzi
wa kike wa Stashahada Mwaka wa Pili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini, Kituo cha Mwanza, akielezea kuhusu mafunzo wanayoyapata chuoni
hapo na namna elimu hiyo inavyosaidia kuendeleza vijiji walivyokwenda
kufanya mazoezi kwa vitendo mkoani Mwanza, wakati Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) alipotembelea na
kukagua maonesho hayo ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na chuo
hicho.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto),
akionesha moja ya machapisho yaliyotolewa na Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini wakati alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma,
huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829
katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo
cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto),
akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkufunzi wa Chuo
cha Mipango na Maendeleo Vijijini Bw. Ezekiel Kanire, (aliyeshika
kipaza sauti) wakati alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma,
huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829
katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo
cha Mwanza. Kushoto kwa Dkt. Kijaji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (Mb).
No comments:
Post a Comment