• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 6 December 2016

    RC MAKONDA ATEMBELEA HOSPITALI YA CHANIKA JIJINI DAR ES SALAAM


    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefanyaziara kukagua mradi wa Hospitali ya Mama na Mtoto uliopo Chanika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa mradi huo ukikamilika Mwezi Februari 2017 utaondoa hadha kwa wakazi wa maeneo ya jirani ambao walilazimika kwenda kupata huduma Hospitali ya Amana na Muhimbili.rc-makonda-chanika-6

    RC Makonda amefafanua kuwa Hospitali hiyo itakuwa na vitanda takribani 160 na uwezo wa kuhudumia zaidi ya wagonjwa 1000 kwa siku, huku ikiwa na vyumba viwili vya upasuaji vyenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa wanne kwa kila chumba kimoja, na kuongeza kutakuwa na watumishi zaidi ya 150 ambao watakuwa na makazi yao hapohapo.rc-makonda-chanika-16

    Katika hatua nyingine RC Makonda amewaomba wafadhili wa mradi huo ambao ni Shirika la Maendeleo la Nchini Korea (KOICA) kusaidia upatikanaji wa mradi kama huo katika Wilaya za Ubungo na Kigamboni ambapo utasaidia wakazi wengi walio nje ya mji kupata huduma za Afya, Mradi huo wa  Hospitali ya Mama na Mtoto kwa Chanika unataraji kugharimu takribani bilioni 8 na milioni 800, huku endapo mradi wa Ubgungu na Kigamboni ukifanikiwa utagharimu zaidi ya bilioni 17.


    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI