Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Baraza la
Waislamu Nchini BAKWATA Hamis Mataka amewataka wazazi kuwachunga watoto
na kuhakikisha wanakuwa na maadili mema kwani ulimwengu umebadilika
wanaweza wakapandikizwa vitu vitakavyo kuwa na athari hapo baadae, hivyo
wakichungwa na kupatiwa elimu bora yenye utambuzi wataishinda vita
hiyo.
Mwenyekiti huyo akimuwakilisha Muft wa
Tanzania Abubakar Zubeir ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika
mahafali ya 5 ya shule ya Msingi IBUN JAZARY iliyopo wilaya ya Mkuranga
Mkoani Pwani na kusisitiza kuwa kwa mujibu ya Dini ya Kiislamu maadili
na tabia njema humjenga muislam jambo ambalo shule hiyo inalifanya na
kuwapelekea wanafunzi kuishi kwa kumuogopa Mungu.
Pia ameipongeza shule hiyo kwa kuweza
kutoa Elimu ya Dini na Dunia pamoja jambo ambalo shule zingine hazifanyi
na kufafanua kuwa kufanya hivyo ni kumpa mwanafunzi akili ya yale
anayojifunza na moyo wa kumuogopa Mwenyezi Mungu kwa kufanya yaliyo
mema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule
hiyo Othman Ally Kaporo amewashukuru wadau wote waliochangia mafanikio
ya shule kwa kuwa shule bora kwa Mkoa wa Pwani kwa kutoa kumi bora ya
wanafunzi kimkoa jambo ambalo limempelekea kutowatoza ada tano bora ya
wanafunzi hao watakao endelea na shule ya Sekondari inayomilikiwa na
taasisi hiyo ya Ibun Jazary.
No comments:
Post a Comment