Mashambulizi mawili ya kujilipua mabomu yametokea nje ya uwanja wa soka wa club ya Besiktas ambayo inashiriki ligi kuu ya Uturuki siku ya Jumamosi usiku sana.
Milipuko hiyo imetoka nje ya uwanja wa soka masaa mawili baada ya mechi kuisha wakati hata wachambuzi wakiwa bado wanaendelea kuchambua mechi na mashabiki hawajatawanyika wote vizuri.
Ripoti zinasema mabomu hayo yaliwalenga mapilsi ambapo kati ya 38 waliokufa 30 ni mapolisi na 8 kuwa ni raia wa kawaida hasa mashabiki wa soka. Watu 155 walikimbizwa hospitali na wengine 14 walipelekwa chumba cha ICU.

No comments:
Post a Comment