Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji yafungua kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Rwanda katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji (EPZA) uliopo Ubungo External. Kongamano hilo limefunguliwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia. Edwin Amandus Ngonyani (Aliyemwakilisha Waziri wa Viwanda) na Mhe. Waziri wa Biashara, Viwanda na Masuala ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda Mhe. Francois Kanimba.
Aidha, Leo tarehe 08 Desemba, 2016 kutakuwa na mkutano wa pamoja (bilateral meeting) kati ya Tanzania na Rwanda kuanzia saa nne kamili asubuhi (04:00) katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Mkutano huo utaongozwa na waheshimiwa Mawaziri kutoka pande zote mbili (Tanzania na Rwanda).
No comments:
Post a Comment