• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 9 December 2016

    WIZARA YALAANI BINTI KUCHUNWA NGOZI WILAYANI KARATU, ARUSHA

    tanzania
    Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inalaani vikali kuchunwa ngozi mtoto Witness Andrew (9) ambaye alitekwa wakati akichunga mifugo na kuokotwa akiwa amefariki dunia wilayani Karatu katika Mkoa wa Arusha, mapema wiki hii.
    Wizara imesikitishwa na mauaji ya binti huyo, ambaye uhai wake umekatishwa na watu wasiojulikana wakati akiwa katika wajibu wa kuwasidia wazazi kufanya kazi ndogo ndogo katika familia yake. Mauaji haya ni ukatili wa hali ya juu na ni kiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi ya mtoto ambayo ndiyo haki ya msingi kati ya haki zote za mtoto. Haki ya kuishi inapovunjwa ndani ya jamii inatia doa jamii husika katika kujenga jamii zinayofaa kuwa mahali salama kwa Mtoto kuishi.
    Wizara inaamini kuwa, Mamlaka zinazohusika na ulinzi wa Mtoto dhidi ya ukatili katika Mkoa wa Arusha hususan Wilaya ya Karatu, zitahakikisha watuhumiwa wanasakwa na kukamatwa ili sheria stahiki iweze kuchukua mkondo wake.
    Inasikitisha kuwa mauaji ya mtoto yametokea kipindi ambacho Taifa linaadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia duniani. Miongoni mwa vitendo vinavyopigiwa kelele ni kuacha imani na desturi zenye madhara ikiwemo imani ya ushirikina katika jamii zetu.
    Kwa kutambua hili, tarehe 13 Desemba, 2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto itazindua Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili. Mpango huu ambao ni jumuishi unalenga kuendeleza juhudi za Serikali na wadau katika shirikiana pamoja kuzuia ukatili na kutoa huduma stahiki kwa wahanga wa ukatili nchini.
    Wizara inatoa pole kwa wazazi, ndugu, familia, marafiki, wanafunzi na walimu wa mtoto Witness Andrew ambaye ameuawa katika umri mdogo na tunawaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
          Erasto T. Ching’oro

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI