• Breaking News

    ..

    ..

    Friday, 20 January 2017

    ADC wahitimisha kampeni za udiwani kijichi

    Moja ya maneno mazuri ambayo mwenyekiti wa chama cha ADC Hamadi  Rashid aliyazungumza katika kampeni za mwisho za uchaguzi mdogo ngazi ya Diwani kata ya kijichi jijini Dar es salaam ambapo Mama Nuru ndiye mgombea kupitia chama hicho.
    Mwenyekiti huyo amesema lengo kuu la chama chake ni kuwatoa watu katika umaskini na kutatua shida mbalimbali kwakuwa uongozi na jopo zima la ADC linahofu na Mungu.
    Ametoa misimamo yake mbalimbali  haswa kwa kiongozi aliyeko madarakani atawajibishwa kama akikosea kabla ya wananchi kumuwajibisha katika uchaguzi mkuu, pamoja na yote amewataka viongozi wa chama hicho kuacha maneno na kufanya kilicho wafanya waombe kula.
    Asilimia 70 vitendo na asilimia 30 ndio maneno kwa ajiri ya kuwajulisha watu mambo mbalimbali, katika kampeni hiyo Hamad Rashid ameomba na kuwashauri wakazi hao kujiunga na vikundi mbalimbali ili waweze kupatiwa elimu kisha watapewa fedha kwa ajiri ya vikundi hivyo kwa maana ya vikoba,  tayari ameagiza vikubdi vya watu 30 wakae pamoja na wakiwa tayari watoe taarifa ila mipango ifanyike. Baada ya mkutano kuisha wanachama mbalimbali wamejiunga  na chama hicho.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI