• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 4 January 2017

    BAADA YA ZIARA YA WAZIRI MKUU KATIKA KIWANDA CHA WATERCOM, WAMEAMUA KUSEMA HAYA

    Siku ya jana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasim Majaliwa alifanya ziara katika wilaya ya Kigamboni na kutembelea maeneo kadhaa ikiwemo Kiwanda cha Maziwa na Maji cha Watercom na Milkcom ambapo aliwaomba watanzania kununua bidhaa za wazawa kwani zinakuza uchumi wa ndani.pm-majaliwa-1
    Kufuatia ziara hiyo ya Waziri Mkuu kiwanda mojawapo cha Watercom kupitia msemaji wao Abubakari Faraji wameeleza walichojifunza kupitia ziara hiyo ya Waziri Mkuu na kusema kuwa wanaipongeza serikali ya awamu ya tano kwani iko tayari kufanyakazi na wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza, na kufafanua kuwa Waziri Mkuu amewaomba kutumia fursa ikiwemo eneo la Longido ambapo kuna ng'ombe wengi ambao wanaweza kuwatumia kwaajili ya uzalishaji wa maziwa na kupanua soko lenye kukuza ajira.watercom-3

    Kuhusu kuzitumia fursa hizo Msemaji huyo Abubakari Faraji ameeleza kuwa watazithamini na kuzifanyia kazi, akieleza mafanikio ya viwanda hivyo kwa pamoja ameeleza kuwa wanazalisha takribani milioni lita za maji na lita 240,000 za maziwa kwa siku, na kueleza kuwa kiwanda kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 1800 na endapo changamoto za umeme na miundombinu zitafanyiwa kazi wataajjiri wafanyakazi wengi zaidi hivyo wanaomba serikali iendelee kuwaunga mkono, na wao wataendelea kuwa karibu zaidi na jamii kama walivyojenga wodi ya kisasa kwenye Zahanati ya Kisarawe II.waziri-mkuu

    Jiunge nasi 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI