• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 5 January 2017

    DC TANGA AINGILIA KATI MGOGORO WA WAFUGAJI NA MWEKEZAJI WA SHAMBA LA MKONGE MARUNGU

    dre
     Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa mkutano wa
    wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano
    yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati
    ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa
    mara.
     Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga(DAS),Faidha Salim akizungumza katika mkutano huo
     Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea akizungumza wakati wa mkutano huo
     Mkuu
    wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa katikati akiandika baadhi ya
    maswali ya wananchi ambao walikuwa wakiuliza kwenye mkutano huo.
     Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu huyo wa wilaya.


    MKUU wa
    Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameingilia kati mgogoro wa wafugaji na
    mwekezaji wa shamba la mkonge la Marungu Mkoani Tanga na kutoa miezi mitatu kwa
    wafugaji hao kuhakikisha wanaondoka katika shamba hilo kabla ya serikali haijatumia
    nguvu ya kuwahamisha.


    Akizungumza
    katika kikao cha wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na
    mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano
    yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati
    ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.


    Maamuzi
    hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lililotolewa siku chache
    zilizopita na Mh;WAziri MKuu la kuwataka Wakuu wote wa Wilaya nchi nzima kuhakikisha
    wanamaliza migogoro ya ardhi iliyondani ya uwezo wao ili kutoa fursa kwa
    wananchi kuendelea na shughuli zao.


    Mwilapwa
    alisema kumekuwepo na madhara mengi yanayojiketokeza kutokana na kuwepo kwa
    migogoro ya wakulima na wafugaji hadi kufikia kutokea mapigano yanayohatarisha
    amani iliyopo baina ya makundi hayo mawili jambo ambalo serikali imejidhatiti
    kumaliza migogoro hiyo kwa makubaliano ya mazungumzo.


    “Kumekuwepo
    na mapigano ya mara kwa mara baina ya wakulima,mwekezaji na wafugaji jambo linalovunja
    amani na hata kuhatarisha maisha ya watu nisema ikiwa makubaliano haya
    hayatatekelezwa basi Serikali itaingilia kati na itawahamisha wafugaji hao kwa
    nguvu”Alisema Mwilapa.


    Kwa
    upande wa Diwani wa kata ya Marungu Mohamed Mwambea alisema kuwepo kwa wafugaji
    hao katika shamba hilo ndani Kijiji hicho kumeleta madhara makubwa kutokana na
    kutokea mapigano  kwa pande hizo mbili na
    kutokea uharibifu wa mazao ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo Kijijini
    hapo.


    Mwambea
    alisema imekuwa kawaida kwa wafugaji kushinda katika kesi zao dhidi ya wakulima
    jambo linaloshangaza wanapata wapi haki ya kuweza kushinda kila aina ya kesi
    zinazojitokeza baina ya wakulima na wafugaji.


    “Ifike
    wakati kwa Serikali iwe inatenda haki kwa wakulima dhidi ya wafugaji ili
    kujenga usawa kwa jamii hizo mbili ambazo zinaingia katika migogoro
    inayohatarisha maisha yao na hata jamii inayotuzunguka”Aalisema Mwambea.


    Nae Meneja
    wa shamba la mkonge la Marungu Casmir Joackim alisema wameshindwa kuendelea na
    uzalishaji katika shamba hilo kwa zaidi ya miaka miwili kutokana kuingiliwa na
    wafugaji hao waliohamishia shughuli zao za kifugaji na makazi katika shamba
    hilo.


    Joackim
    alisema dhamira ya muwekezaji wa shamba hilo ni kutekeleza agizo la Serikali ya
    awamu ya tano ya kuwataka wawekezaji wote nchini wayaendeleze mashamba yao
    kiuzalishaji na hata kutoa ajira kwa wananchi ili kukwepa mkono wa Serikali
    unaoweza kufuta hati ya umili wa shamba hilo na kurudishwa serikalini kwa ajili
    ya kugawiwa upya wananchi.


    “Ikiwa
    ndani ya shamba letu wapo wafugaji wanaendelea na shughuli zao za ufugaji
    pamoja na maisha kwa ujumla tangu mwaka 2014 ni namna gani tunaweza kundeleza
    shughuli zetu,huoni mkono wa Serikali unaweza kutukumba lazima tutendewe haki
    kwa hawa watu ambao ni wavamizi”Alisema Joackim.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI