
Wakitoa kero zao mbele ya RC Makonda akiwemo Jacob Anyandwile ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Madereva Tax Ilala, amesema madereva hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutozwa kodi kubwa na mamlaka ya mapato nchini TRA, pia uwepo wa huduma ya Tax kwa njia ya mtandao unafanywa na kampuni ya UBA wameeleza umewaharibia soko kwani kampuni hiyo inatoza bei ndogo zaidi, pia gharama za uendeshaji hazilingani wanajikuta wao wanalipa kodi kubwa zaidi kuliko UBA.

Huku kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja huo Ramadhani Ashiru ameeleza kuwa kampuni hiyo ya UBA inatumia Tax bubu ambazo hazitambuliki kisheria, pia madereva wengine wamezitaja kero nyingine ikiwemo uwepo wa bajaji nyingi kinyume na utaratibu, machinga kupanga bidhaa zao barabarani jambo linalowapelekea kutofika kwa wakati maeneo wanayo wapeleka abiria, pia wamewashushia lawama askari wa barabarani kwa kuwaandikia ‘notification’ hata kwa yale makosa ya kiufundi ambayo yanawatokea wakiwa njiani ikiwemo kuungua kwa ‘bulb’ (taa).

Baada ya kusikiliza kero hizo RC Makonda ameeleza kuwa adhima ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuboresha huduma za usafiri na kuwa za kipekee kama nchi alizozitembelea na kushuhudia huma bora za usafiri ikiwemo Marekani na Afrika ya Kusini, hivyo ameeleza ili huduma za usafiri ziwebora bila kumnyonya mdau yeyote lazima makadirio ya ulipaji ya TRA yaangaliwe ili Tax zilipekiwango kutokana na kazi wanayoifanya, pia huduma za uendeshaji za UBA na madereva Tax ziangaliwe ili kila mtu alipekulingana na stahiki ya kazi yake.

Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo RC Makonda ameeleza kuwa ni vyema kukawepo kifaa maalum kitakacho onesha umbali wa mteja anapokwenda ili alipe kulingana na umbali huo na ajue bei hiyo kuliko kukadiriana, pia amesema katika kufanikisha hayo serikali yke itaziondoa Tax bubu zote, na utaratibu wa kuweka rangi na namba kwenye magari utarudi ili Tax zote zitambulike.

Pia amewasisitiza kutoa taarifa za matukio ya kiharifu pale wanapomuhisi abiria waliyempakia na kuongeza kuwa wakifanya hivyo watalisaidia Taifa kuwa katika hali ya usalama, huku akiwataka ndani ya wiki moja wakae wajadiliane waje na mapendekezo yatakayokuwa na tija kwa pande zote.

No comments:
Post a Comment