Kulikuwa na taarifa iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba Wakaazi wa Jumbi, Wilaya ya kati Unguja wiki mbili baada ya mazishi ya mtu mmoja wamegundua kuwa mtu aliezikwa yupo mtaani na anaonekana katika mazingira ya kutatanisha, na hivyo kuamua kwenda kulifukua kaburi na kukutana na majanga hayo hapo kama picha zinavyoonesha.
Tulipolifuatilia suala hili kwa undani zaidi inasemekana taarifa hizo hazikuwa na ukweli ila taarifa iliyo sahihi ni kwamba
Taarifa ya kufukuliwa kaburi imetokea Bungi na sio Jumbi kama ilivyodaiwa.
Hata hivyo hakuna mtu aliekufa na kuzikwa kisha kuonekana mitaani kama taarifa zinavyosema.
Kilichotokea ni kwamba wametokea watu wasiojulikana wameenda porini kisha kuchimba shimo mfano wa kaburi na kuzika vitu vinavyosadikiwa kuwa vya ushirikina.
Shimo lilifukuliwa chini ya usimamizi wa Polisi na maafisa wengine wa kiserikali na hakupatikana mtu aliezikwa hapo.
No comments:
Post a Comment