Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amemteua Bw.Yusuph Singo Omari kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kujaza nafasi iliyo achwa wazi na Bw Leornad Thadeo aliyehamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 kifungu namba 6(1)(b) kikisomwa pamoja na kifungu namba 8 cha sheria hiyo.
Kabla ya uteuzi huo Bw.Yusuph Singo Omari alikuwa Mkufunzi Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Ardhi katika masuala ya Michezo.
Mhe.Nape Moses Nnauye pia amemshukuru aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wote Bw. Alex Nkenyenge ambaye alifanya kazi zake kwa uadilifu na kujituma kwa kusimamia majukumu yote ya Idara kwa ukamilifu.
Aidha ametoa wito kwa wanamichezo na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Bw Yusuph Singo Omari atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.
Imetolewa na:
Zawadi Msalla
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
No comments:
Post a Comment