Serikali mkoani Geita ,imesema
kuwa itahakikisha inaboresha zao la pamba kwa kutumia viadudu ambavyo
vitasaidia kunusuru pamba kwenye maeneo ya vijijini ambako wakulima
wengi wanaendelea kulima.
Akizungumza kwenye kikao cha
wadau wa zao la Pamba kilichofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Mkoa na
kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Wilaya zote za mkoa wa Geita
wakiwemo Maafisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika pamoja na Wakuu wa Bodi
ya Pamba kanda ya ziwa,
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,amesema kuwa pamoja na hali ya
changamoto ya ukame na mvua kunyesha kwa uchache bado wakulima
wameitikia wito na kulima hali ambayo kwa sasa inatia matumaini
kutokana na pamba kuoto vizuri vijijini.
“Huko vijijini wamaenza
kulalamika kutokana na upungufu wa viuadudu sasa na sisi hapa lazima
tupate uvumbuzi kwamba hili tatizo la viuadudu tunalipatia majibu sahihi
ambayo yatawasaidia wakulima wetu kule vijijini, wakulima wameitikia
vizuri pamoja na hali hii ya mvua ambazo sio kamilifu, mvua ni chache,
mvua ni haba lakini wakulima wameitikia” alibainisha mh kyunga
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe
akiwemo Emily Kasagara Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa
Geita na Safari Mayala Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe
wameelezea changamoto dhidi ya zao la pamba na kusema kuwa.
“Kuna changamoto mbalimbali
zilizojitokeza kuhusiana na zao hli la pamba, moja ni kuwa wakulima
wengi walielekeza nguvu zaidi kwenye mazao ya chakula kipindi mvua
zilipoanza kunyesha na badala ya zao la pamba kwa hiyo ndio maana hata
katika taarifa yetu kile kilimo cha pamba kiliextend mpaka mwezi Januari
kwa sababu mvua zilipoanza kunyesha tu wakawa wamerash kulima mazao ya
chakula lakini baadae sasa wakalima zao letu la pamba ambalo limeenda
mpaka Januari” alisema
Aidha katika msimu wa mwaka
2016-2017 Mkoa ulilenga kulima jumla ya tani elfu sitini na saba na
mbili (67,002) zilizotarajiwa kutoa mavuno ya tani elfu tisini na tatu
mia nne thelathini na saba (93,437) lakini changamoto ya mvua za vuli
kutonyesha vizuri katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Geita imeweza
kusababisha malengo hayo kutokufikiwa

No comments:
Post a Comment