• Breaking News

    ..

    ..

    Monday 27 February 2017

    Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni imeagizwa kuhamisha kiasi cha shilingi milioni 132




    Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni imeagizwa kuhamisha kiasi cha shilingi milioni 132 zilizotengwa kwa ajili ya Kuboresha soko la Mkunguni ktk kata ya Hananasifu lenye mgogoro usiokwisha na kuzipeleka kuboresha soko la maandazi ambalo halina mgogoro ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

    Kati ya Fedha hizo shilingi milioni 37 zilitengwa kupitia bajeti ya manispaa ya mwaka 2014/2015 na shilingi milioni 95 ktk bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kuboresha soko hilo.

    Akitoa agizo hilo wakati akizungumza na watendaji wa kata ya Hananasifu Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ALI HAPI ameiagiza manispaa hiyo kuandika barua haraka ktk ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI ili kuomba kibali cha kuhamisha fedha hizo kabla ya mwezi Desemba na kupelekwa pasipo na mgogoro ktk soko la maandazi.


    HAPI ameeleza kuwa haiwezekani fedha za serikali zipelekwa kwenye maeneo yenye migogoro wakati kuna maeneo hayana migogori na yanashindwa kupata maendeleo kwa kukosa fedha za kutekeleza miradi.

    Kwa upande wake mtendaji wa kata hiyo ya Hananasifu SALUM MZAGANYA awali akizungumzia kuhusu Mgogoro wa soko hilo unaokwamisha shughuli za maendeleo amesema,  Unahusisha pande tatu ushirika wa soko hilo na Manispaa ya Kinondoni ambapo kila upanse unadai ni eneo lake huku wananchi wanaomiliki viwanja sita ndani ya soko wanadai soko limejengwa ndani ya viwanja vyao.

    Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ametembelea na kukagua soko hilo na kuutaka ushirika wa soko, wananchi wanaomiliki viwanja hapo na manispaa kuwa na kamati ya pamoja kwa ajili ya kuweka mambo sawa na serikali ipeleke fedha kwa ajili ya kuendeleza soko hilo kwani kuna fedha zilitengwa kwa ajili hiyo lakini zitahamishiwa sehemu nyingine kutokana na mgogoro uliopo.

    Katika ziara yake hiyo HAPI pia ametembelea soko la maandazi,  zahanati ya hananasifu pamoja na shule ya sekondari Hananasifu.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI