










i
BODI YA UHARIRI
Mwenyekiti
Dkt.Hassan Abbasi Mkurugenzi-Idara ya Habari-MAELEZO
Wajumbe
Zamaradi KawawaVicent Tiganya John Lukuwi Patrick KipangulaElias Malima
Wasanifu Jarida
Benedict LiwengaHassan Silayo
Huduma zitolewazo MAELEZO
1. Kuuza picha za Viongozi wa Taifa na matukio muhimu ya Serikali,2. Kusajili magazeti pamoja na majarida,3. Kukodisha ukumbi kwa ajili ya mikutano na Waandishi waHabari,4. Rejea ya magazeti na picha za zamani,5. Kupokea kero mbalimbali za Wananchi
Jarida hili hutolewa na
Idara ya Habari-MAELEZO S.L.P 8031Dar es Salaam, Simu: 022-2122771Baruapepe: maelezo@habari.go.tz Tovuti: tanzania.go.tz
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

TAHARIRI
Tanzania ni NCHI YETU na kwa faida yetu
Wapendwa wasomaji wa jarida hili la NCHI YETU lenye historia ndefu naTanzania yetu, ninayo furaha leo, mimi binafsi na timu nzima ya Idara yaHabari-MAELEZO, kushuhudia historia nyingine ya jarida hili kuanza kutokamtandaoni.Kama inavyofahamika, kwa miaka mingi sasa jarida la NCHI YETU limekuwalikichapishwa na nakala zake kusambazwa wakati wa maadhimisho makubwaya kitaifa tu kama vile sherehe za Muungano na Uhuru.Wakati tukiahidi kuwa machapisho hayo maalum ya siku hizo yataendelea, nifaraja kwetu leo kuona jinsi maendeleo ya teknolojia na mageuzi katika sektaya upashanaji habari, yanavyotuwezesha kulichapisha jarida hili kwa njia ya
mitandao ili kuwakia wasomaji wengi zaidi.
Hivyo basi, kuanzia Januari, 2017, ukiacha matoleo maalum, jarida lako hililitakuwa likitoka kila mwezi kwa njia hii na tutajitahidi kulisambaza kwa njia
mbalimbali mitandaoni ili kuwakia wasomaji wengi.
Tunawaahidi kuwa NCHI YETU litabaki kuwa jarida lile lile lililosheheni habarina uchambuzi muhimu kuhusu maendeleo na jitihada za nchi yetu Tanzaniapamoja na watu wake katika kujiletea maendeleo. Jarida litasheheni piamatukio muhimu yaliyotokea katika mwezi husika na litakumbushia pia historiaya nyuma.NCHI YETU pia litakuwa johari muhimu ya kuhamasisha utii kwa tunu muhimuza Taifa letu kama vile amani, utulivu, uzalendo, lugha na utamaduni. Ni jarida litakalosimama na kusimamia Tanzania tunayoitaka, na itakapobidi,tutakemea na kuonya juhudi zozote za kuzifuta tunu hizi.Ndio maana tahariri hii ya kwanza imeanza kwa kutukumbusha jambomuhimu-kwamba Tanzania ni nchi yetu na sote tuna budi na dhima yakuchangia katika maendeleo yake kwa faida yetu ya sasa lakini na vizazivijavyo.Nawatakia usomaji mwema wa jarida hili. Asanteni sana.
Dkt. Hassan Abbasi,Mwenyekiti, Bodi ya Uhariri,Mkurugenzi-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali
ii
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

No comments:
Post a Comment